Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, mjini Morogoro, leo. Waziri Lugola amewatuliza madereva wa vyombo vya moto waliotaka kugoma kutokana na kutopewa mikataba ya kazi, matumizi mabaya ya tochi pamoja na ulipaji wa faini na kusimamishwa hovyo na matrafiki mabarabarani. Lugola mewataka wamiliki wa vyombo vya moto nchini kutoa mikataba ya kazi kwa madereva na wafanyakazi mbalimbali katika makampuni yao. Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akifurahi jambo wakati alipokua anamsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Nchini, Chuki Shaban alipokuwa akizungumza katika kikao cha Wadau wa usafirishaji kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, mjini Morogoro, jana. Waziri Lugola amewatuliza madereva wa vyombo vya moto waliotaka kugoma kutokana na kutopewa mikataba ya kazi, matumizi mabaya ya tochi pamoja na ulipaji wa faini na kusimamishwa hovyo na matrafiki mabarabarani. Kushoto ni Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, mjini Morogoro, leo. Waziri Lugola amewatuliza madereva wa vyombo vya moto waliotaka kugoma kutokana na kutopewa mikataba ya kazi, matumizi mabaya ya tochi pamoja na ulipaji wa faini na kusimamishwa hovyo na matrafiki mabarabarani. Lugola mewataka wamiliki wa vyombo vya moto nchini kutoa mikataba ya kazi kwa madereva na wafanyakazi mbalimbali katika makampuni yao. Kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim. Wapili kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
……………….
Na Felix Mwagara, (MOHA) Morogoro
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewatuliza madereva wa vyombo vya moto nchini waliotangaza kufanya mgomo wiki iliyopita wakilalamikia kutopata haki zao mbalimbali.
Madereva hao wanalalamikia kutopewa mikataba ya kazi, matumizi mabaya ya tochi kwa askari wa usalama barabarani, ulipaji wa faini wa uonevu na kusimamishwa hovyo na askari mabarabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, Mjini Morogoro, Waziri Lugola alisema Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ni sikivu, baada ya kupata malalamiko yako ya kutaka mgomo, viongozi hao wamekutana ili kupata suluhisho ya malalamiko yao.
Lugola alisema kabla ya kuzungumza na waandishi hao, walifanya kikao Mei 18, 2019 na wadau wa usafirishaji nchini, ambao ni Chama cha Wamiliki wa Mabasi, Wamiliki wa Malori, Chama cha Madereva wa Malori, Chama chja Madereva Mabasi na Chama cha Madereva wa Madalala.
Waziri Lugola ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde, Wawakilishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), na Jeshi la Polisi, walikubaliana na viongozi wenzake kukutana tena kwa ajili ya kupata suluhisho ya baadhi ya malalamiko ya wadau hao ikiwemo lalamiko la kudhibiti mwendo.
“Serikali ya Rais Dkt. Magufuli ni sikivu ndiyo mana tumekutana hapa, tunawaagiza wamiliki wa vyombo vya moto nchini kutoa mikataba ya kazi kwa madereva na wafanyakazi mbalimbali katika makampuni yao, tochi zipigwe kjwa weledi na si kuwaonea madreva kwakutoonekana picha ya gari lililofanya kosa, kusimishwa hovyo barabarani pamoja na kutosimamisha mabasi ambayo yana abiria.
Lugola ameongeza kuwa, mgomo wa aina yoyote ni ukiukwaji wa Sheria za nchi hivyo ni marufuku kufanya jaribio hilo ambalo lilitishiwa kufanywa.