Home Mchanganyiko VIJANA WILAYANI MUHEZA WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VIDOGO

VIJANA WILAYANI MUHEZA WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VIDOGO

0

 KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Kata ya Mlingano wilayani Muheza Waziri Mohamed ambaye pia ni
Katibu wa
Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Tanga

KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Kata ya Mlingano Jimbo la Muheza wilayani Muheza Waziri Mohamed amewataka vijana wilayani humo
kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Magufuli.

 

 

Waziri ambaye pia ni Katibu wa
Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Tanga aliyasema hayo wakati
aliofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mlingano Jimbo la
Muheza aliyoijenga kwa kutumia kiasi cha milioni 7.4
Kwa mujibu wa Katibu huyo ameamua kujenga ofisi hiyo
kutokana na kwamba kata hiyo kutokuwa nayo kwa muda mrefu na hivyo kuona haja
ya kuhakikisha ujenzi huo unafanyika ili kuwawezesha viongozi kutekeleza wajibu
wao wa kukijenga chama hicho.
Aidha alisema pia iwapo vijana
watatumia muda wao kufikiria namna ya kujikita kwenye uanzishwaji wa viwanda
hivyo utawasaidia kuweza kujiajiri na kuweza kuisaidia jamii kwa kutoa ajira
kwa wenzao na hivyo kuchangia pato la mkoa na Taifa kwa ujumla.
“Lakini pia vijana wenzangu tuunge
mkono juhudi za serikali kwa kushiriki kwenye miradi ya kimaendeleo
inayotekelezwa kwenye maeneo yetu kwa kujitoa na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji
maendeleo katika jamii zinazotuzunguka “Alisema.

 

Muonekano wa Jengo la Ofisi ya CCM kata ya Mlingano wilayani Muheza
ambalo limejengwa na KATIBU Mwenezi wa Kata ya Mlingano Jimbo la Muheza
ambaye pia ni Katibu Hamasa Chipukizi wa UVCCM Mkoa wa Tanga Waziri
Mohamed Waziri kwa asilimia 90 ambapo mpaka kukamilika kwake ametumia
kiasi cha milioni 7.4