Home Michezo RAIS KARIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA ZFA KUFUATIA KIFO CHA...

RAIS KARIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA ZFA KUFUATIA KIFO CHA RAIS WA ZAMANI ALI FEREJI TAMIMU

0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa Familia,Ndugu,jamaa,marafiki na Chama Cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa ZFA Ali Fereji Tamimu.
Katika salamu hizo za rambirambi Rais wa TFF Ndugu Karia amemuelezea Marehemu Tamimu kama mmoja wa Wanamichezo waliotoa mchango mkubwa katika Mpira wa Miguu hususani Visiwani Zanzibar.
“Ni ukweli usiofichika Marehemu Tamimu alikua na mchango mkubwa katika Mpira wa Miguu wa Tanzania hususani Zanzibar ambako amekua kiongozi kwa miaka kadhaa,Kwa niaba ya TFF natoa pole kwa Familia,Ndugu,Jamaa,Marafiki na ZFA ambayo amewahi kushika wadhifa wa juu kabisa” amesema Karia.
Ameongeza kuwa katika kipindi hiki kigumu TFF inaungana na Wafiwa pamoja na Wanamichezo wote.
Marehemu Ali Fereji Tamimu enzi za uhai wake mbali ya kuongoza katika nafasi ya juu ya Rais wa ZFA,pia amewahi kuwa Kiongozi wa Baraza la Vyama na Vilabu Afrika Mashariki na Kati CECAFA na amewahi kuwemo kwenye Kamati mbalimbali.
Atazikwa leo saa 10 jioni kwenye Makaburi ya mwanakwerekwe Zanzibar.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.