Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tawla) Mkoani Tanga Wakili Latifa Mwabondo akizungumza jambo wakati wa uanzishwaji wa klabu za Ardhi kwenye shule za Sekondari Magila na
Kilulu wilayani Muheza uliofanywa na Chama cha Wanasheria wanawake mkoani Tanga (TAWLA) kupitia mradi wao kupata, kutumia, kumiliki na kufanya maamuzi kwa wanawake kwenye masuala la ardhi utawasaidia kuondoa vikwazo vilivyopo kwenye jamii.
Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tawla) Mkoani Tanga Wakili Latifa Mwabondo akizungumza jambo wakati wa uanzishwaji wa klabu
za Ardhi kwenye shule za Sekondari Magila na
Kilulu wilayani Muheza uliofanywa na Chama cha Wanasheria wanawake
mkoani Tanga (TAWLA) kupitia mradi wao kupata, kutumia, kumiliki na kufanya maamuzi kwa wanawake kwenye masuala la ardhi utawasaidia kuondoa
vikwazo vilivyopo kwenye jamii
Afisa Sheria kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Mkoani Tanga (TAWLA) Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo wakati wa uanzishwaji wa klabu
hizo
MKUU wa Kitengo cha Sheria Halmashauri ya wilaya ya Muheza Aisha Mhando akisisitiza jambo
Afisa Sheria kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Mkoani Tanga (TAWLA) Mwanaidi Kombo kulia akimsikiliza kwa umakini Mratibu wa Chama hicho Mkoani Tanga Wakili Latifa Mwabondo wakati wa uanzishwaji wa klabu
hizo
Mratibu wa Chama hicho Mkoani Tanga Wakili Latifa Mwabondo kulia akimueleza kitui Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Magila wilayani Muheza |
Sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo wakifuatilia kwa umakini
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Magila wakifuatilia kwa umakini
Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Wakili Latifa Mwabondo aliyevaa kilemba cha njano akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya uzinduzi wa klabu hiyo wa kwanza kulia aliyesimama ni Afisa Sheria kutoka TAWLA mkoani Tanga Mwanaidi Kombo
Uanzishwaji wa klabu za Ardhi kwenye shule za Sekondari Magila na Kilulu wilayani Muheza uliofanywa na Chama cha Wanasheria wanawake mkoani
Tanga (TAWLA) kupitia mradi wao kuwezesha upatikanaji haki za wanawake katika kumiliki,kupata,kutumia na kufanya maamuzi juu ya ardhi ma mali umeelezwa kwamba utawasaidia kuwapa uelewa na kuondosha vikwazo vilivyopo kwenye jamii.
Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Magila wilayani Muheza mkoani Tanga Kibwana Senkopwa wakati uanzishwaji wa klabu za Ardhi shuleni hapo ambapo alisema wanafunzi hao watanapopata elimu hiyo ya sheria itawasaidia kuweza kusaidia jamii zao kwa kutoa elimu hususani changamoto zinazojitokeza.
Alisema vikwazo hivyo vitaondoka kutokana na kwamba wakati mwengine kutokana na kukosekana kwa elimu kwenye jamii imekuwa ni vigumu sana kwa wanawake kwenye changamoto zinatokana na umiliki wa ardhi kwenye maeneo yao wanayoishi.
“Kwani leo hii tumepewa malengo na faida hivyo itatusaidia sisi kuweza kuvuna elimu ya sheria ambayo sasa itakuwa ni chachu kubwa kuweza kuisaidia jamii na hivyo kusaidia kupunguza vikwazo vinavyowakabili wanawake kwenye jamii”Alisema.
Aidha alisema pia hatua hiyo itakuwa mwarobaini wa vikwazo ambavyona jamii nyingi imekuwa ikikutana navyo kutokana na kutokujua sheria hususani juu ya upatikanaji wa haki ya kumiliki ardhi kwa wanawake jambo ambalo limepelekea asilimia kubwa kunyanyasika kwenye jamii zao.
Awali akizungumza katika halfa hiyo ya uundwaji wa klabu hizo, Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tawla) Mkoani Tanga Wakili Latifa Mwabondo alisema mradi huo unafanyika mkoa wa Tanga kwenye Kata za Kilulu na Magila.
Alisema wanafunzi waliochaguliwa watapatiwa mafunzo juu ya haki izo ili kuweza kueneza elimu kwa wanawake katika maeneo yao ikiwa ni katika kupambana na changamoto wanazozipata wanawake katika maeneo mengi hasa vijijini
“Klabu hizi zitaweza kuwa chachu kubwa kuweza kutoa elimu kwa jamii masuala la ardhi na hivyo kuwa msaada mkubwa kwenye kukakabiliana na vikwazo vinavyokuwa vikijitokeza katika maeneo yao “Alisema
Alisema baada ya wanafunzi hao kupata mafunzo hayo yatawawezesha kuweza kuwa na uelewa juu ya sheria na baadae kuweza kuielimisha jamii kuhusu sheria za ardhi jambo ambalo litaweza kuondoa fikra zilizopo.
Naye mwanafunzi wa kidato cha tatu kwenye shule hiyo ambao wamechaguliwa kwenye klabu hiyo Rashid Kivugo alisema uwepo wao huko utawasaidia kuwaimarisha na kuwajengea uwezo mkubwa wa kuweza kutambua masuala ya
kisheria.
Mwisho.