Bw. Peter Chuwa Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Bandarini akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za (WMA) zilizopo kwenye Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam leo wakati akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu vipimo vya mafuta kwenye Meli Kwenye Matanki ya kuhifadhia na kwenye maroli yanayosafirisha nishati hiyo hapa nchini na nchi mbalimbali. |
Bw. Peter Chuwa amesema kuna umuhimu mkubwa sana kupima mafuta katika hatua yoyote ile iwe kwenye meli , kwenye matanki na hata kwenye maroli yanayosafirisha ili walaji waweze kupata ujazo ulio sahihi kabisa na wauzaji pia wauze kwa viwango na vipimo vinavyostahili na vilivyothibitishwa.
Mei 20 mwaka 1875 makampuni kadhaa huko ufaransa yalikutana na kujadili kuhusu vipimo hivyo ambapo yalikipitisha kipimo cha ujazo wa mita baada ya hapo tarehe ya Mei 20 kila mwaka iliteuliwa kuwa siku ya vipimo na imekuwa ikiadhimishwa duniani kote, Siku ya Jumatatu Mei 20,2019 ya wiki ijayo maadhimisho hayo yatafanyika jijini Dar es salaam.
Mjasiriamali na Mbunifu wa mashine mbalimbali za kutengenezea sabuni
Bw. George Butafwe akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wa TBC wakati wanahabari hao walipotembelea
katika karakana yake iliyopo (SIDO) jijini Dar es salaam leo.
Bw. George Butafwe akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wa TBC wakati wanahabari hao walipotembelea
katika karakana yake iliyopo (SIDO) jijini Dar es salaam leo.
Afisa Vipimo II, Joram Joshua akiwa melini kwa ajili ya kupima ujazo wa mafuta Bandalini kabla hayajaanza kushushwa kwenye meli .