Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kushoto) akiwasili katika Viwanja vya NaneNane, Mkoani Morogoro tayari kwa Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Mei 17 – 18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu akihutubia katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Mei 17 – 18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Mei 17 – 18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Wakuu wa Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu(hayupo pichani).
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Usalama, Mhe. Salum Rehani(vazi la kiraia) akiongea katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara, leo Mei 17, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Magereza toka katika vituo mbalimbali nchini(waliosimama) baada ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara, leo Mei 17, 2019. Wa pili toka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike(Picha na Jeshi la Magereza).