Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akisaini kitabu cha maombolezo wakati wa kuaga miili mitano ya waliokuwa wafanyakazi wa Kituo cha Linunga cha Azam Media kilichoko Tabata Relini jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi hao walifariki katika ajali ya gari mkoani Singida jana asubuhi wakati wakielekea Chato mkoani Geita ambako wangerusha moja kwa moja matangazo ya uzinduzi wa mbuga ya wanyama ya Burigi iliyoko Chato mkoani Geita leo ambayo imezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Viongozi mbalimbali wa serikali, Vyama vya Siasa Mashirika na Taasisi mbalimbali wakiwasili katika ofisi za Azam Media tayari kwa kushiriki kuaga miili ya waliokuwa wafanyakazi wa kituo hicho waliofariki kwa ajali mkoani Singida jana.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na Mbunge wa zamani wa Bukoba mjini na Balozi. Khamis Kagasheki katika msiba huo kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Picha zikionyesha viongozi mbalimbali wakijadiliana mawili matatu wakati wakisubiri kuwasili kwa miili ya wafanyakazi wa Azam Media kwa ajili ya kuaga.
Magari maalum yaliyobe miili ya waliokuwa wafanyakazi wa Azam Media yakiwasili kwenye ofisi za Azamn Media kwa ajili ya kuagwa rasmi kwa miili hiyo ili kuendelea na taratibu za mazishi katika maeneo mbalimbali marehemu hao watakakozikwa.
Waombolezajimbalimbali wakisimama wakati miili ya wafanyakazi hao ikiwasili.
Baadhi ya waombolezaji mbalimbali wakilia kwa uchungu baada ya miili hiyo kuwasili katika ofisi za Azam Media Tabata Relini leo.
Waombolezaji mbalimbali wakibeba majeneza ili kuyapanga vizuri tayari kwa waombolezaji kuaga.
Majeneza yenye miili ya waliokuwa wafanyakazi wa Azam Media yakiwa yamepangwa vyema tayari kwa shughuli ya kutoa heshima za mwisho.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Deodatus Balile akizungumza wakati akitoa salam za pole kwa ndugu jamaa na marafiki waliopatwa na msiba huo.
Wabunge wanawake mbalimbali wameshiriki kutoa heshima za mwisho wa marehemu hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV Joyce Mhavile akitoa salamu za pole kwa wana Azam Media na dugu jamaa na marafiki kwa kufikwa na msiba huo mkubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC Dk. Ayoub Ryoba akitoa salamu za pole pia.
Mkurugenzi Mtendaji wa TCRAMhandisi .James Kilaba akitoa salamu za pole kwa familia na ndugu jamaa na marafiki pamoja na Azam Media.
Katibu Mwenezi wa CCM Ndugu Humprey Polepole akizungumza katika msiba huo.
Mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe naye ametoa pole kwa wafiwa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na kutoa salam za pole kwa wafiwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Injinia Hamad Yusuf Masauni akitoa salam za pole kwa wafiwa kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na MichezoDk. Harisson Mwakyembe akizungumza na kutoa salam za pole kwa wafiwa kwa niaba ya wizara ya habari.
Mkurugenzi wa Azam Media Tido Mhando akizungumza wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa waliokuwa wafanyakazi wa Azam Media waliofariki jana kwa ajali ya gari mkoani Singida.