MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na
Makamu Mwenyekiti wa UWT Bi. Thuwaiba Editon Kisasi, alipowasili katika
viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar kuhudhua Dua ya
kuiombea Nchi Amani ilioandaliwa na UWT Zanzibar
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akitia ubani
katika chetezo kuashiria kufungua kisomo cha Dua ya kuitakia Amani Nchi
kipindi cha Uchaguzi na baada ya uchaguzi iliofanyika katika ukumbi wa
Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, ilioandaliwa na UWT
Zanzibar. na (kushoto kwa Mama) Makamu Mwenyekiti wa UWT Bi.Thuwaiba
Editon Kisasi , Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mama
Maryam Mwinyi,Mke wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Asha Bilal
na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Bi Leila Ngozi na (kulia kwa Mama) Mke wa
Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Zakia Bilal, wakihudhuria kisoma hicho
kilichofanyika 26/10/2020.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akitia ubani
katika chetezo kuashiria kufungua kisomo cha Dua ya kuitakia Amani Nchi
kipindi cha Uchaguzi na baada ya uchaguzi iliofanyika katika ukumbi wa
Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, ilioandaliwa na UWT
Zanzibar. na (kushoto kwa Mama) Makamu Mwenyekiti wa UWT Bi.Thuwaiba
Editon Kisasi , Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mama
Maryam Mwinyi,Mke wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Asha Bilal
na (kulia kwa Mama) Mke wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Zakia
Bilal, wakihudhuria kisoma hicho kilichofanyika 26/10/2020
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akijumuika na
Wananchi wa Zanzibar katika kisomo cha Dua kuiombea Nchi Amani wakati wa
Uchaguzi na baada ya Uchaguzi ilioandaliwa na U WT katika ukumbi wa
Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, na (kulia kwa Mama) Mke wa
Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Siti Mwinyi, Mke wa Makamu wa Rais Mstaaf
Mama Zakia Bilal na (kushoto kwa Mama) Makamu Mwenyekiti wa UWT Bi.
Thuwaiba Editon Kisasi, Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mama Maryam
Mwinyi, Mke wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Asha Bilal na
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Bi Leila Ngozi, wakitikia dua ya kuhitimisha
kisomo hicho ikisomwa na Bi. Fatma Mliwa iliofanyika jana
26/10/2020
BAADHI ya Wananchi wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa
kisoma cha Dua kuiombea Nchi Amani ilioandaliwa na UWT, iliofanyika
katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.jana
26/10/2020.(Picha na Ikulu)