Home Michezo SUPER D AMNOWA VICENT MBILINYI KUMKABILI SHEDRACK IGNAS NOVEMBA 28 MASAKI

SUPER D AMNOWA VICENT MBILINYI KUMKABILI SHEDRACK IGNAS NOVEMBA 28 MASAKI

0

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ akimfundisha bondia Vicent Mbilinyi kupiga ngumi yenye mkunjo wa chini ‘UPCAT’ kwa ajili ya maandalizi yake na Shedrack Ignas litakalofanyika Novemba 28 katika ukumbi wa Nexrt Door Arena

 Na Mwandishi wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi yupo katika maandalizi mazito sana katika kujiandaa kwake kwa mpambano wake na Shedrack Ignas utakaofanyika Novemba 28 katika ukumbi wa Nextri Door Arena Masaki Dar es salaam

akizungumza wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na pambano hilo Mbilinyi amesema kuwa yeye ngumi ni kazi yake hivyo anaiheshimu kwa kufanya mazoezi kwa bidii na wakati muhafaka kabisa kwani ndio moja na yaisha yake ya kila siku

alivyo ulizwa amejipangaje kumkabili bondia Shedrack Ignas ambaye ni mgumu pia ni nunda kwa uvumilivu wa ngumi hapa nchini

amesema ajakutana na ngumi kali hivyo ajipange kwa kipigo kitakatifu ambacho atampatia bila huruma yani hakika katika ngumi nimejifunza mambo mengi hususani nilivyokwenda safari za nje hivyo siwezi kukubali kupigwa kizembe na kwa uraisi hapa Tanzania

Nae kocha wake ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema kwamba ana shaka na bondia wake huyo kwani yupo fiti na mtiifu wa mazoezi hivyo ushindi kwake kama kumsukuma mlevi kwani ngumi ni kipaji nae anacho hivyo anatumia kipaji