Home Mchanganyiko KAMATI YA AMANI YA VIONGOZI WA DINI MKOA WA DODOMA WAKUTANA KUSISITIZA...

KAMATI YA AMANI YA VIONGOZI WA DINI MKOA WA DODOMA WAKUTANA KUSISITIZA KUDUMISHWA KWA AMANI KATIKA UCHAGUZI MKUU.

0

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dodoma Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Askofu Amon Kinyunyu wakiwaongoza Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma kutoa tamko kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuwataka wanachama na viongozi wa siasa kutunza na kulinda Amani siku ya Uchaguzi Mkuu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dodoma Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu, akiongoza Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma kutoa tamko kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuwataka wanachama na viongozi wa siasa kutunza na kulinda Amani siku ya Uchaguzi Mkuu.

Afisa Programu wa Mahusiano ya Dini mbalimbali toka Jumuiya Kikristo Tanzania CCT Mchungaji Daudi Kalinga,akitoa taarifa wakati wa Tamko la Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini  kuelekea  uchaguzi Mkuu hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

 Baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Amani ya Dini Mkoa wa Dodoma wakifatilia hotuba ya  Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu akitoa  tamko kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuwaasa wananchi kulinda Amani siku ya kupiga kura.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dodoma Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Askofu Amon Kinyunyu wakiwaongoza Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma kuliombea Taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuwataka wanachama na viongozi wa siasa kutunza na kulinda Amani siku ya Uchaguzi Mkuu.

Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma wakiliombea Taifa  kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuwataka wanachama na viongozi wa siasa kutunza na kulinda Amani siku ya Uchaguzi Mkuu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dodoma Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu  na Makamu Mwenyekiti wake Askofu Amon Kinyunyu wakiwa katika picha ya pamoja na  Viongozi wa Dini wa kamati ya Amani Mkoa wa Dodoma mara baada ya  kutoa tamko kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuwataka wanachama na viongozi wa siasa kutunza na kulinda Amani siku ya Uchaguzi Mkuu.

……………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October 28 mwaka huu Kamati ya Viongozi wa Dini mkoa wa Dodoma wamekutana na kutoa tamko huku wakipinga aina yoyote ya vurugu na maandamo,viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kujitokeza wakati wa uchaguzi huo.

Pia kamati hiyo imewataka watanzania  kujitokeza kupiga kura kwa utulivu bila kufanya vitendo vya uvunjifu amani ili kuenzi amani ya Taifa ambayo ni tunu ambayo tumetunukiwa na Mungu.

Akitoa tamko hilo leo jijini Dodoma  Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajab kwa niaba ya kamati hiyo ambapo amesema jukumu la ulinzi wa amani ni la kila mtanzania kwani endapo amani itapotea watakaoumia ni watanzania wenyewe.

Sheikh Rajab amesema wao kama kamati ya amani ya Mkoa wanashangazwa na kusikitishwa na viongozi wa Dini ambao kwa nyakati tofauti wamesahau majukumu yao na kujitokeza kwenye kampeni za kisiasa kuwanadi wagombea pamoja na kuhamasisha vijana kujitokeza kufanya maandamano jambo ambalo linachochea uvunjifu wa amani.

Amewasihi vijana kutokubali kutumika na wanasiasa na watakapopiga kura warejee majumbani mwao na wasihadaishwe na wagombea wanaowataka kubaki kwenye vituo vya kupiga kura kulinda kura kwani jukumu la kulinda kura lipo mikononi mwa mawakala wa vyama pamoja na tume ya uchaguzi.

” Sisi kama viongozi wa dini ni jukumu letu kukemea vitendo vya uvunjifu amani na kuhamasisha wananchi ambao ndio waumini wetu kuwa watulivu, tuwaombe mkapige kura kwa amani na kurudi majumbani, msishawishike wala kuhadaiwa,” Amesema Sheikh Rajab.

Amewaasa wazazi na walezi kwenye kila familia kuwaasa vijana wao kujiepusha na kila aina ya vishawishi kwenda kuandamana na kufanya fujo kwa sababu mwisho wa siku watakabiliwa ba sheria za nchi na wale waliokua wakiwahamasisha hawatokua nchini watakua wamekimbia nchi.