Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga akiangalia baadhi ya teknolojia zilizobuniwa na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Maonesho ya biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam
************
NA EMMANUEL MBATILO
Gavana Luoga amewapa pongezi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuwashirikisha wanafunzi hasa kuonesha ujuzi na maalifa ambao wameupata Vyuoni kwani unaweza kuwasaidia kutengeneza utatuzi wa matatizo ya kijamii kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga katika Maonesho ya biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
“Kama wanafunzi wanaweza wakawa ndio wanaonyesha jinsi gani wanatumia maalifa waliyoyapata ili kuweza kutengeneza vitu ambavyo vinatatua matatizo ya jamii na kutumiwa na jamii hiyo ni faida kubwa sana”. Amesema Prof.Luoga.
Aidha, Prof.Luoga ametoa wito kwa wananchi kupenda kutumia elimu ama maalifa ambayo yanazalishwa Vyuoni kwani vyuo visibaki kuzalisha maalifa ambayo hayatumiki ambapo vitu vingi ambavyo vinazalishwa na Chuo vinaweza kutumika na wananchi.