Home Michezo MANE AIPELEKA SENEGAL ROBO FAIANALI AFCON,BENIN YAING’OA MOROCCO KWA MATUTA

MANE AIPELEKA SENEGAL ROBO FAIANALI AFCON,BENIN YAING’OA MOROCCO KWA MATUTA

0

TIMU za Senegal na Benin zimefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi dhidi ya wapinzani wao Morocco na Uganda Ijumaa.
Mshambuliaji wa Liverpool ya England, Sadio Mane ndiye aliyeipeleka Robo Fainali Senegal kwa bao lake la dakika ya 15 akimalizia pasi ya  M’Baye Niang wa Rennes ya Ufaransa, kwa kuwatoka mabeki wa The Cranes, Juuko Murshid na Hassan Wasswa.
Kipa wa Denis Masinde Onyango wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini akapangua mkwaju wa penalti Mane dakika ya 61 kuinyima Senegal bao la pili.
Katika mchezo uliotangulia, Benin iliibuka na ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Morocco kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Al Salam mjini Cairo.

Beki wa Levadiakos ya Ugiriki, Moise Adilehou alianza kuifungia Benin dakika ya 53 kabla ya mshambuliaji wa Leganes, Youssef En-Nesyri kuisawazishia Morocco dakika ya 75.
Kiungo wa Ajax ya Uholanzi, Hakim Ziyech akaikosesha ushindi timu yake baada ya kukosa penalti dakika ya 90 na ushei na mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza.
Benin ikapata pigo dakika ya 97 baada ya beki wake, Abdul Khaled Akiola Adenon anayechezea Amiens SC ya Ufaransa kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi yap ii ya njano kwa kukaidi maamuzi ya refa.
Kipa wa Benin, Owalabi Saturnin Allagbe Kassifa anayedakia klabu ya Niort ya Daraja la Pili, Ufaransa akapangua penalti mbili za kiungo wa Southampton, Sofiane Boufal nay a mshambuliaji wa Leganes, Youssef En-Nesyri.
Waliofunga penalti za Benin ni Olivier Verdon wa Deportivo Alaves, David Djigla wa Niort, Tidjani Anaane wa Ben Guerdane ya Tunisia na Seibou Mama wa Toulon ya Ufaransa, wakati Oussama Idrissi wa AZ ya Uholanzi ndiye pekee aliyefunga penalty ya Morocco.