Home Michezo Erick Rutanga aongeza miaka miwili kuitumikia Rayon Sport

Erick Rutanga aongeza miaka miwili kuitumikia Rayon Sport

0

**************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Rayon Sports imemuongeza mkataba wa miaka miwili beki wa kushoto wa timu hiyo Erick Rutanga ambaye alikuwa akitajwa kuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa wakiwaniwa na Yanga kuchukua nafasi ya Gadiel Michael.

Awali klabu ya Nkana Fc ilijitosa kumuwania beki huyo mahiri, hata hivyo hawakufikia muafaka.

Yanga inaweza kumsajili beki wa zamani wa Singida United ambaye msimu uliopita aliichezea Gor Mahia Shafiq Batambuze kuchukua nafasi ya Gadiel ambaye amepewa ruhusa ya kujiunga na timu anayotaka.