Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma wakati alipotangaza kuanza kwa awamu ya tau ya kampeni za chama hicho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Humphrey Polepole akisisitiza jambo akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma wakati alipotangaza kuanza kwa awamu ya tau ya kampeni za chama hicho.
(NA JOHN BUKUKU-DODOMA)
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Humphrey Polepole wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma wakati alipotangaza kuanza kwa awamu ya tau ya kampeni za chama hicho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Humphrey Polepole amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeingia awamu ya tatu ya Kampeni zake na Mgombea Urais wa chama hicho Dkt.John Magufuli ataanza kufanya kampeni zake Nyanda za juu Kusini akianzia Mkoani Iringa kesho na kuendelea mkoani Mbeya.
Ameongeza kuwa katika awamu hii ya tatu itawatumia Marais wastaafu akiwemo Rais wa ya Pili,Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Kikwete na Mawaziri wakuu katika Kampeni zake ya ndani ya siku 30 zilizobaki.
Polepole amesema wameamua kuongeza injini nyingine wakiwemo viongozi wa juu wa Chama hicho na kufanya mashambulizi makubwa ya siasa katika kufanya siasa safi za kistaarabu zitakazojikita katika kueleza hoja na ilani ya chama chao.
Amesema Mgombea wa Urais wa Chama hicho anaanza rasmi awamu ya Tatu kufanya mikutano yake kwa Mkoa wa Iringa na Mbeya awamu hii atatumia kuwaeleza watanzania juu ya maono yake kwa nchi na maono ya kisera na kiilani katika muhula wake wa pili wa kuomba dhamana kwa watanzania katika kuongoza kwa muhula mwingine.
Akizungumza na waandishi leo Polepole amesema ndani ya siku 30 zilizobakia kampeni za Chama hicho zitaongozwa na Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt.John Magufuli,Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassan,Mjumbe wa halmashauri kuu ambaye pia ni Mjumbe wa kamati kuu Kassim Majaliwa ,Makada waandamizi wa CCM, pamoja na Mawaziri wakuu wakuu wastaafu.
“Watanzania waendelee kutarajia kupata ujumbe wa kuimarisha amani na maono yao wanapotaka kuipeleka Tanzania chini ya Dkt.Magufuli pamoja na kuhakikisha kudumisha Mshikamano na amani ambayo inalindwa,inatunzwa na kuienzi kwa wivu mkubwa,”Ameongeza.
Siku 30 kufikia Oktoba 27, 2020 siku ya mwisho ya kupiga kampeni kabla ya Oktoba 28,2020, tunasisitiza watu wenye mapenzi mema kwa nchi kutumia siku hiyo kupiga kura kwa kishindo kwa Mgombea urais wa CCM Rais Dk. Magufuli,sambamba na wagombea ubunge na udiwani ili kukamilisha utatu wa Chama hicho”amesema Polepole.
Aidha Chama kimelitaka Jeshi la Polisi kufanya haraka kwa uchunguzi wa kifo cha Mwenyekiti wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa ,Imanueli Mlelwa kilichotokea hivikaribuni Mkoani Iringa baada ya kupigiwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa akiwa amefariki.
“Uchaguzi huu unaendeshwa kwa sheria za uchaguzi,kanuni zake na maadili ya vyama serikali na Tume ambapo vyama vyote vimeridhia na kuweka saini ila tunashangaa wenzetu tunapofika karibia ya uchaguzi wanazungumza kuhusu vurugu na kutoa maneno ya uongo,”amesema