Home Michezo YANGA YAZIDI KUNOGA,YAICHAPA MTIBWA SUGAR BAO 1-O KWENYE UWANJA WA JAMHURI MJINI...

YANGA YAZIDI KUNOGA,YAICHAPA MTIBWA SUGAR BAO 1-O KWENYE UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO

0

********************************

EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuondoka na pointi tatu baada ya kufanikiwa kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Timu zote mbili zilikwenda mapumziko zikiwa hazijafungana japo Yanga iliweza kutawala mchezo na kujaribu kutafuta nafasi biloa mafanikio.

Kipindi cha pili Mchezo ulizidi kuwa wa aina yake baada ya timu zote kuonesha anahitaji ushindi katika mchezo huo ambao ulijawa na hisia kali za mashabiki wa pande zote mbili.

Yanga ilifanikiwa kupata bao kupitia kwa beki wao kisiki raia wa Ghana Lamine Moro baada ya kutendea vyema kona iliyopigwa na Kiungo Mshambuliaji raia wa Angola mwenye asili ya Kireno Carlos Guimares Carlinhos.