Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika moja ya mikutano yake ya kampeni.
(NA JOHN BUKUKU-DODOMA)
Mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Tundu Lissu
………………………………………….
Miongoni mwa mataifa makubwa yanayoishi kwa kusimangana na kukinzana kiutawala kati ya majimbo yake na serikali kuu mbali ya kuwa makubwa kiuchumi, kijamii na kidiplomasia basi ni Marekani.
Hii ni kutokana na wakati mwingine utofauti wa sheria za majimbo na serikali kuu lakini pia kipato baina ya jimbo na jimbo, kila jimbo linajiona ni kubwa zaidi ya wenzake, huku mengine yakijinasibisha na umiliki wa taifa hilo.
Marekani iliamua kujiunga na kuwa na mfumo wa majimbo kwa lengo la kujiukuza kiuchumi, mawazo yao yalikuwa mazuri lakini hawakutazama mbali na ndiyo maana si ajabu kuona watu wa nchi moja hawalingani kiuchumi.
Itakumbukwa katika miaka ya mwanzoni mwa nchi za Kiafrika kujinyakulia uhuru wake, kulikuwa na mkutano mkubwa nchini Ghana, chini ya uenyekiti wa aliyekuwa rais wa nchi ya Ghana, Kwame Nkrumah.
Majadliano ya mkutano huo yalikuwa ni kuangalia namna ya kuziunganisha nchi za kiafrika, kuunda umoja wa Afrika. Lakini baadhi ya viongozi akiwemo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hawakuafikiana na wazo hilo, sababu walizotoa ni za msingi kabisa kuwa Afrika ilihitaji muda ndipo nchi ziungane.
Mwalimu Nyerere aliona mbali, alijua ni lazima kwanza nchi zijitawale na kuweka usawa katika namna ya upatikanaji rasilimali ili jimbo moja lisiwe kubwa zaidi ya lingine. Kwa sababu kungekosekana usawa na kuwafanya baadhi kuwa wanyonge na baadhi kujiona ni wakubwa.
Mawazo ya Mwalimu Nyerere ilikuwa ni kutafuta muungano wa nchi chache zilizo jirani ili kuangalia kama kuungana kwao kutakuwa na tija. Ndipo mwaka 1967ulipoanzishwa muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)ambao hata hivyo haukufanikiwa baada ya kuvunjika mkwaka 1977 kabla ya kuanzishwa tena mnamo Januari 2001.
Tukiangalia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliojumuisha nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda ni masuala ya kimaslahi. Kila nchi ilijiona inastahiki kuheshimika zaidi ya nyingine kutokana na utofauti wa kipato na mchango katika jumuiya.
Kilichotakiwa ni kuzifanya nchi hizo baadaye ziwe kama majimbo, kuwepo na sarafu moja, pasi moja ya kusafiria na masuala ya kimkakati ikiwemo kuwana rais mmoja.
Utaona kilichofanya EAC kuvunjia ni yale yale ambayo kwa sasa Marekani wanakutana nayo, laiti utakwenda kufanya utafiti kwenye majimbo kadhaa ya taifa hili kubwa, utakutana na malalamiko mengi juu ya utaratibu huo unaokandamiza baadhi na kuinua baadhi.
Msingi wa hoja hizi nilizozitanguliza hapo juu ni mawazo ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demkrasiana Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu kutaka Tanzania ianze kuwa na mfumo wa majimbo.
Yaani kuangalia namna ya kuwa na uongozi wa kimafungu, kila mkoa uwe jimbo linalojitegemea au kila kanda iundwe kuwa jimbo linalojitegemea.
Kitu hicho hakiwezekani kwa Tanzania ya sasa ambayo inatengenezwa kwa kutumia rasilimali za asili pamoja na fedha zinazokusanywa kupitia Utalii, Madini, Bandari na biashara mbalimbali.
Mathalan, Mkoa wa Dar es Salaam ndio unaoongoza kwa mapato Tanzania, kwa sababu kuna bandari, wafanyabiashara wakubwa wanaochangia kipato cha taifa pamoja na uwanja mkubwa wa ndege ambao unapokea wageni wengi kutoka kila pembe ya dunia.
Ukiangalia baadhi ya mikoa inayotoka Kaskazini mwa nchi kuna utajiri wa madini pamoja na utalii.
Hata hivyo, kuna baadhi ya maeneo hayana rasilimali za kutosha kama vile kanda ya kati na baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini. Lakini bado inatakiwa Tanzania iwe na muingiliano wa kijamii.
Majimbo yanatengeneza matabaka, kila jimbo litajiona lina hadhi ya juu kuliko jimbo jingine.
Lakini pia kiutawala kila jimbo litakuwa na sheria zake zinazotawala ndani ya jimbo ambazo huenda pia zikakinza na sheria za serikali kuu jambo ambalo litapelekea mtawala wa serikali kuu au sheria za serikali kuu kushindwa kudhibiti baadhi ya majimbo kiutawala kwa sababu yatakuwa nanguvu ya kiuchumi na pia kisheria.
Ndiyo maana mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni rais wa nchi Dk. John Magufuli mara kwa mara anarudia kauli yake kuwa utaratibu wa majimbo utaturudisha nyuma.
Utatupeleka kwenye mawazo ya kikoloni ambayo walikuwa na lengo la kuigawa nchi ili kila ene liwe na uongozi wake wa kikabila na kikanda.
Katika mikutano yake mingi rais Dk.Magufuli amekuwa akisema waziwazi kuwa Serikali ya majimbo itatusambaratisha na kuligawa taifa ambalo kwa sasa ni moja na maendeleo yake yanakwenda kwa pamoja.
Anatolea mfano wa wazi kabisa kwamba ndiyo maana fedha za madini ya dhahabu kutoka mkoani Geita zinakwenda kujenga barabara mkoa wa Lindi, Fedha za Utalii kutoka Arusha zinakwenda kujenga vituo vya afya mkoani Katavi na Fedha za Korosho kutoka mtwara zinakwenda kununua madawa yanayosambazwa nchi nzima ili kuwahudumia watanzania.
Huo ndiyo mfumo mzuri wa kiutawala ambao mapato ya nchi yanakwenda kuwanufaisha watu wote waliomasikini na walio na kipato kikubwa.