…………………………………………………………..
Na Allawi Kaboyo Bukoba.
Jeshi la zima moto na uokoaji Wilayani Ngara Mkoani Kagera limefanya uokozi wa Mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kuanzia siku 0-3 baada kutupwa kwenye shimo la choo cha zahanati ya Mshikamano iliyopo wilayani humo.
Akizungumzia tukio hilo Kwa waandishi wa habari mjini Bukoba Kamanda wa jeshi hilo Inspector Hamiss Dawa ameeleza kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya asubuhi na wao wamepata taarifa hizo kutoka kwa jeshi la polisi.