WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’ yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu tamisemi (Afya) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Dk Doroth Gwajima,akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’ yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’ yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Taasisi ya chakula na lishe Tanzania(TFNC) Dkt. Germana Leyna,akitoa taarifa wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’ yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’ yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akizindua Piramid ya Lishe ambayo imebeba makundi matano ya chakula wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’ yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akipata maelezo kutoka kwa Afisa Lishe Mtafiti Rose Msaki mara baada ya kuzindua Piramid ya Lishe ambayo imebeba makundi matano ya chakula wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’ yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akipata maelezo Afisa Mtafiti Mwandamizi Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bi.Neema Joshua juu ya chakula wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’ yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi mara baada ya kumaliza kuzungumza kwenye maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’ yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imepinga marufuku utoaji wa vidonge vya Asidi ya Foliki kwa wanafunzi au wasichana balehe badala yake viendelee kutolewa kwa wajawazito na wanawake walio katika umri wa kuzaa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yenye kauli mbiu ‘mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana’.
Ummy amesema kuwa ni marufuku kuwapa wanafunzi na wasichana balehe vidonge vya asidi ya foliki, badala yake fedha hizo zinazotolewa kwa ajili ya dawa hizo, zitumike kuanzisha bustani shuleni ili kuzalisha vyakula vinavyotoa madini hayo.
“Mbali na kuanzishwa kwa bustani shuleni lakini pia fedha hizo zinaweza kupelekwa kwa vijana ili waanzishe miradi ya bustani za mboga kwa ajili ya kuzalisha mazao yanayozalisha asidi hiyo yakiwemo maboga, matunda na hata karoti badala ya kutoa vidonge kwa wanafunzi,” amesema Ummy.
Kuhusu unywaji wa maziwa shuleni, Waziri Ummy amesema kuwa atamwandikia barua ya pendekezo Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako ili kuanzia Septemba mosi mwaka huu kila shule iwe na kibanda cha maziwa kwa ajili ya wanafunzi.
Aidha amesema kuwa utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaonesha kwamba kila mtu anatakiwa kunywa nusu lita ya maziwa sawa na lita 180 kwa mwaka, lakini kwa sasa kila mtu anakunywa lita 40 kwa mwaka sawa na vijiko 10 vya chai kwa siku.
Kuhusu udumavu wa watoto wa chini ya miaka mitano amesema umepungua kutoka asilimia 34.4 mwaka 2014 hadi asilimia 31.8 mwaka juzi,licha ya kuwa jitihada zinataakiwa kuendelea kuchukuliwa.
Naye Naibu Katibu Mkuu tamisemi (Afya) Dk Doroth Gwajima amesema fedha ambazo zinatengwa Sh 1,000 kwa kila halmashauri kwa ajili ya kuimarisha lishe ya watoto zimekuwa zikiongezeka.
Dk Gwajima amesema, fedha hizo zilianza kutengwa 2017/18 ambapo zilipatikana Sh bilioni tisa na zikatumika asilimia 30 tu, 2018/19 zilitengwa Sh bilioni 15 zikatumika asilimia 45.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amesema kuna mabadiliko makubwa kwa wananchi ya kupungua ukondevu.
Odunga amesema kuwa juhudi zinatakiwa ili kuhakikisha siku 1,000 za tangu kutungwa mimba kwa mtoto hadi kuzaliwa afya kwake mama anazingatia kula vyakula ambavyo vinatakiwa kwa afya ya mama na mtoto.
Awali Mkurugenzi wa Taasisi ya chakula na lishe Tanzania(TFNC) Dkt. Germana Leyna amesema kuwa udumavu kwa watoto Tanzania upo chini ya asilimia 30,Unene asilimia 30,upungufu was damu kwa wajawazito asilimia 30 na Unene wastani wa asilimia 30.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Maadhimisho ya Siku ya Lishe yatafanyika kila Agosti 7, kila mwaka, pia atamwandikia Waziri Mkuu kuomba ahamishwe ili yasiiingiliane na Nanenane katika maadhimisho ya mwakani ambapo yataadhimishwa hadi ngazi ya vijiji.