ALIYEKUA Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dodoma, Deo Ndejembi amerudisha Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Chilonwa lililopo wilayani Chamwino, Dodoma.Fomu hiyo amemkabidhi Katibu wa CCM wilaya ya Chamwino Eva Jordan.
ALIYEKUA Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dodoma, Deo Ndejembi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Chilonwa lililopo wilayani Chamwino, Dodoma.
…………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
ALIYEKUA Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dodoma, Deo Ndejembi amemshukuru Rais Dk John Magufuli kwa kumuamini katika nafasi ya u-DC kwa miaka minne pamoja na kumpa ruhusa ya kwenda kugombea Ubunge.
Ndejembi ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati alipokua akirudisha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Chilonwa lililopo wilayani Chamwino, Dodoma.
Amesema ilikua ni bahati kubwa kuaminiwa na Rais Magufuli katika serikali ya awamu ya tano ambayo imejipambanua ndani na nje ya Nchi kwa uadilifu wake wa kuwatumikia watanzania pamoja na kuiletea Nchi maendeleo.
” Ni bahati kubwa sana kufanya kazi na Kiongozi mwenye maono makubwa kama Rais Magufuli, namshukuru sana kwa kuniamini ndani ya miaka minne hii, ninajivunia kuwa sehemu ya mabadiliko ya serikali yetu ambayo imeleta maendeleo chanya ya Nchi yetu.
Ninakwenda kugombea Ubunge Jimbo la Chilonwa ili pia nitumie nguvu na akili zake kusukuma maendeleo kwa wananchi kuwa kushirikiana na serikali,” Amesema Ndejembi.
Ndejembi ametoa shukrani kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa kwa ushirikiano mkubwa aliompa katika kuwatumikia wananchi wa Kongwa pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa, Katibu Tawala na wananchi wote wa Kongwa kwa kushirikiana nae kwa miaka yote minne.
” Kwa kazi kubwa aliyofanya Rais Magufuli hakika nitakua mstari wa mbele kumpigia kampeni na kueleza mambo mazuri ya maendeleo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano ikiwemo kufanikisha Tanzania kufikia uchumi wa kati,” Amesema Ndejembi.