Home Mchanganyiko MAHAKAMA YA WETE YA MPIGA FAINI YA LAKI TANO OTHUMA KWA KUMSHAMBULIA...

MAHAKAMA YA WETE YA MPIGA FAINI YA LAKI TANO OTHUMA KWA KUMSHAMBULIA MTOTO WA MIAKA 16 ZANZIBAR

0

 

Na Masanja Mabula. PEMBA

MAHAKAMA ya Mkoa  Wete imemtoza faini ya shilingi 500,000 na fidia ya shilingi 200, 000    Seif Othman Khamis (23) mkaazi wa Ndagoni Wilaya Chake Chake   kwa kosa la kufanya shambulio la aibu kwa mtoto mwenye umri wa miaka 16  mkaazi wa  Mtambwe.

Imeelezwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Ali Amour Makame  mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Abdalla Yahya Shamhuna kwamba  kijana huyo alitenda kosa hilo tarehe 10/11/2018  majira ya saa 10:00 jioni huko Kinazini Mtambwe   alimchezea binti huyo,  sehemu za maungo ya siri jambo ambalo ni kosa kisheria.

Aidha   kosa alilotenda  ni kinyume na kifungu cha 114 (1)  sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar,

Endapo atashindwa kulipa faini na fidia hiyo, atalazimika kutumikia kifungo cha miaka miwili katika chuo cha mafunzo.

Wakati huo huo Mahakama hiyo ya Mkoa Wete  mbele ya hakimu huyo imemuachia huru  mtuhumiwa Juma Rashid Daudi   miaka 20 mkaazi wa Majenzi Micheweni anaedaiwa  kumtorosha, na kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17.

 Hayo yalijiri baada ya mashahidi wa upande wa mlalamikaji kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi.

Awali ilielezwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Serikali  Ali Amour Makame kuwa, , Oktoba 29/2019  majira ya 1:00  usiku eneo la Ndaambani wilaya ya Micheweni,  bila ya halali na bila ya ridhaa ya wazazi wake alimtorosha msichana jina  linahifadhiwa,  kutoka nyumbani kwao  na kumpeleka eneo  ambapo  ni kosa kinyume  na kifungu cha 113[a] Sheria nambari 6 ya 2018 cha sheria ya Zanzibar.