Waziri wa Madini Doto Biteko akimjulia hali Mwandishi wa habari wa TBC 1 Nazareth Ndekia aliekuwepo kwenye msafara wa ziara ya waziri huyo Mkoani Kagera.
Waziri wa Madini Doto Biteko akiwajulia hali baadhi ya Waandishi wa
habari walio kaa baada ya kupata ajali waliokuwepo kwenye msafara
wa ziara ya waziri huyo Mkoani Kagera.
…………………………………………………………………………….
Na Issa Mtuwa – WM- Kagera
Waandishi wa Habari Wanne Nazareth Ndekia wa TBC 1, Salma Mrisho wa Star TV, Emmanuel Ibrahim wa Clouds Tv na Victor Bariety wa Channel Ten wa kituo cha Geita wamepata ajali wakiwa kwenye Ziara ya Waziri wa Madini Doto Biteko Mkoani Kagera.
Ajali hiyo imetokea mara baada ya Dereva kuwakwepa watoto na kuacha Barabara na Kuingia mtaroni. Mara baada ya kupata ajali hiyo walikimbizwa kwenye Kituo Cha Afya Mrusagamba.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mrusagamba Benedicto Igulu alisema, majeruhi wote wanaendelea vizuri na wamepatiwa matibabu huku Nazareth Ndekia amepata maumivu kiasi ya Kichwa na Shingo na kwamba amepelekwa Kituo cha Afya Runzewe. Salma Mrisho wa Star TV amepasuka kidevuni na kushonwa nyuzi mbili na anaendelea vizuri huku wengine wawili wamepatiwa matibabu ya kawaida na wote wameruhusiwa.
Mmoja wa Majeruhi Victor Bateiry alisema ajali hiyo ilitokana na uwepo wa watoto barabarani ambapo hawakuona msururu wa Magari ya msafara yaliyokuwepo na kwamba barabara ilikuwa na vumbi sana kiasi cha kuona gari za nyuma kuiona kirahisi.
Ziara hiyo ilikuwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Geita na Kagera.
Waandishi wengine waliokupo kwenye ziara hiyo ni pamoja na Basir Elius wa ITV, Mariam Shabani mwakilishi wa EATV na Azam TV na George Binagi wa BMG. Waandishi walikuwa kwenye magari mawili tofauti.
Wananchi waliosaidia gari hiyo kuiondoa walisema eneo la kona hiyo kumekuwa na ajali kadhaa huku wakisema hata kwenye msafara wa mbio za mwenge siku za nyuma gari imewahi pata ajali kwenye kona hiyo.