Na Sixmund Begashe, Arusha
WIZARA ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi zake za Uhifadhi na Utalii, pamoja na mambo mengine, imeendelea kuutumia vyema Mkutano wa 24 wa Jukwaa la Uhifadhi wa Wanyamapori Barani Afrika (24th African Wildlife Consultanive Forum – 2th AWCF ) kama fursa adhimu na adimu ya kutangaza vivutio vya utalii nchini.
Kupitia Mkutano huo wa Kimataifa unaofanyikia jijini Arusha chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Alexander Lobora ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara hiyo imetumia nafasi mbalimbali za kunadi mazao ya utalii ikiwemo asali ya Tanzania kwa wajumbe hao.
Wajumbe hao wameipenda kazi hiyo nzuri inayofanya na Wizara huku wakiahidi kuwa Mabalozi wazuri wa Tanzania nchini mwao.

