Morogoro

Timu ya Netiboli ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA Queens) imeanza kwa ushindi mashindano ya SHIMMUTA-2026 baada ya kuichapa timu ya IAE kwa magoli 45–23 katika mchezo wake wa kwanza uliochezwa leo katika uwanja wa X Bwalo, mkoani Morogoro.

Katika mchezo huo, TMDA Queens ilionesha kiwango kizuri kwa kuanza kwa kasi, kufanya mashambulizi yenye mpangilio na kuimarisha ulinzi, hali iliyoiwezesha kutawala mchezo na kupata ushindi huo wa magoli 45.

Ushindi huo unaipa TMDA Queens mwanzo mzuri wa safari yake katika mashindano hayo, huku timu hiyo ikiendelea kuwania nafasi ya kutwaa ubingwa wa SHIMMUTA-2026.

TMDA Queens sasa inaelekeza nguvu katika michezo inayofuata kwa lengo la kuendeleza kiwango kizuri na kufanya vizuri katika mashindano hayo.