Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki Ibada ya Misa Takatifu ya kumuombea Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kumbukizi ya Miaka 27 tangu kufariki kwake, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania Jimbo Katoliki Sumbawanga, leo tarehe 14 Oktoba 2026.
Ibada hiyo, imeongozwa na Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo Katoliki Sumbawanga na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere, pamoja na Viongozi, waumini na wananchi mbalimbali.

