*Wajadili mikakati ya kuimarisha upatikanaji wa huduma za nishati vijijini

*Wajipanga kukabiliana na athari za mvua za El Nino na mabadiliko ya gharama za utekelezaji wa miradi

Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Felchesmi Mramba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy, kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu upelekaji wa nishati katika maeneo ya vijijini.

Pamoja na mambo mengine mazungumzo hayo yamejikita katika kujadili mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini, kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma za nishati kwa wananchi na kuhakikisha miradi hiyo inachangia kukuza shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Aidha walijadili kuhusu mikakati ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hususan mvua kunyesha zina zotegemea kuanza za El Nino pamoja na mabadiliko ya gharama za uzalishaji ikiwemo usafirishaji wa vifaa vya ujenzi wa miradi katima soko la dunia.