Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Oktoba 13, 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na Libasse Guèye, Elia Mpanzu aliyetikisa nyavu mara mbili, Morice Abraham, Anicet Oura Pomona na Ismael Touré. Bao pekee la Mashujaa FC lilifungwa na Selemani Bwenzi.
Kufuatia matokeo hayo, Simba SC inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza michezo nane.
Wapinzani wao wa jadi, Yanga SC, wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 18 baada ya kucheza michezo saba.
