Na Sixmund Begashe, Arusha
MAKAMU wa Rais wa Seneti ya Ivory Coast ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Masuala ya Kijamii na Kitamaduni ya Seneti ya nchi hiyo, Mhe. Toure Souleymane, amevutiwa na kazi za Wizara ya Maliasili na Utalii za kutangaza vivutio vya utalii katika Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea Jijini Arusha.
Mhe. Souleymane amefika kwenye banda la Wizara hiyo na kuhudumiwa vizuri na wataalam wa taasisi za Wizara na wadau wa utalii nchini.
Amesema ukarimu wa maafisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Watanzania kwa ujumla ni tunu muhimu ya kuheshimiwa ambayo imemfanya yeye na ugeni wote kujisikia wapo nyumbani na kwamba amependezwa na asali ya Tanzania na kuahidi kurudi tena akiwa na familia yake ili kufurahia vivutio vya utalii nchini.
Banda la Maliasili na Utalii limeendelea kutembelewa na viongozi mbalimbali wanaohudhuria Mkutano huo wa Kimataifa unaojumuisha zaidi ya wageni 2,200.

