Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akizungumza kwenye Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026) Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia. Mkutano huo mkubwa wa kimataifa unawakutanisha viongozi wa Serikali, mawaziri wa afya, wataalamu wa afya, wanasayansi, watafiti na washiriki wa maendeleo kutoka Afrika na duniani.

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha African International Convention Centre (AICC), Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki kwenye Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026) pamoja na kuzindua Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika, tarehe 23 Novemba, 2026.

………… 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania kwa kushirikiana na Nigeria itaandaa mkutano wa kwanza wa Afya ya Wanawake Afrika, utakaofanyika Desemba Mosi, 2026.

Amesema mkutano huo unalenga kuimarisha ufuatiliaji wa maazimio ya kisiasa na uwajibikaji katika utekelezaji wa malengo ya kutokomeza vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na watoto, pamoja na kuimarisha maendeleo ya watumishi wa afya na utoaji wa huduma za afya katika ngazi za jamii.

Akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, Rais Samia amesema ushirikiano huo ni sehemu ya juhudi za kuendeleza utekelezaji wa vipaumbele vya afya ya uzazi, mama, mtoto mchanga, mtoto na vijana barani Afrika.

Ameeleza kuwa mkutano huo utatoa fursa ya kuendeleza dhamira ya viongozi wa Afrika katika kuhakikisha ahadi zilizowekwa kuhusu afya ya mama na mtoto zinatafsiriwa kuwa hatua zinazotekelezeka na matokeo yanayopimika.

Rais Samia ametoa wito kwa nchi za Umoja wa Afrika kuimarisha umiliki wa mipango ya afya na kuhakikisha mikakati iliyowekwa inatekelezwa kwa ufanisi ili kuboresha ustawi wa wanawake, watoto na vijana katika bara hilo. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisalimiana na Mhe. Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha African International Convention Centre (AICC), Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki kwenye Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), tarehe 23 Novemba, 2026.

 Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa na Mhe. Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, kwenye picha na viongozi mbalimbali wanaoshiriki kwenye Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 23 Novemba, 2026.
 Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), Jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 23 Novemba, 2026.
[11/23, 2:39 PM] +1 (515) 682-6947: Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC) Dkt. Jean Kaseya baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha African International Convention Centre (AICC), Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki kwenye Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), tarehe 23 Novemba, 2026. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Julius Maada Bio, Rais wa Sierra Leone baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha African International Convention Centre (AICC), Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki kwenye Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), tarehe 23 Novemba, 2026.

 Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC) Dkt. Jean Kaseya baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha African International Convention Centre (AICC), Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki kwenye Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), tarehe 23 Novemba, 2026.
 Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akizungumza na Mhe. Evariste Ndayishimiye, Rais wa Jamhuri ya Burundi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha African International Convention Centre (AICC), Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki kwenye Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), tarehe 23 Novemba, 2026.