Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepata Kombe katika Mashindano ya SHIMIWI kwa kuwa mshindi wa tatu katika Mchezo wa kurusha mishale maarufu mchezo wa Darts
Afisa Rasilimali Watu, Bi. Neema Massawe ambaye ameiwakilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika mchezo huo, ambapo iliibuka mshindi wa tatu na kukabidhiwa kombe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi, wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete tarehe 7 Oktoba, 2026.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zilizoshiriki Mashindano ya SHIMIWI 2026 yaliwakutanisha Watumishi takribani 3,000 kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali na yalianza rasmi tarehe 25 Septemba, 2026 na kukamilika tarehe 7 Oktoba, 2026 Mkoani Kilimanjaro.

