Mkutano wa Saba wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika katika ukumbi wa The Aga Khan Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 04 hadi 07 Oktoba 2026 umemalizika kwa mafanikio makubwa.

Nchi hizi mbili zimekubaliana kuendeleza ushirikiano wa Ulinzi na Usalama ambao ulianzishwa na waasisi wa mataifa haya, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Julius Kambarage Nyerere na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Msumbiji, hayati Samora Machel.