Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mheshimiwa Saidi Othman Yakubu, akiwasilisha rasmi hati za utambulisho kwa Rais wa Ufaransa, Mheshimiwa Emmanuel Macron, mjini Paris. Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijadili maendeleo ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa, hususan katika sekta ya biashara inayoendelea kukua. Rais Macron pia alimpa Balozi Yakubu salamu za pole azifikishe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mumewe, Marehemu Hafidh Ameir.