Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Nickson Babu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma Kwa Wateja  iliyofanyika katika Ofisi za TANESCO Temeke  zilizopo  Oktoba 5, 2026, Kurasini, Dar es Salaam

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Lucia Renatus, akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma Kwa Wateja  2026 iliyofanyik katika Ofisi za TANESCO Temeke  zilizopo  Oktoba 5, 2026, 

………

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Nickson Babu, amefungua Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 katika mkoa huo, huku akiwataka wafanyakazi kuwa wazalendo na kuwajibika katika kutekeleza majukumu yao ili kuongeza ufanisi na kuboresha huduma kwa wateja.

Akizungumza na wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke katika hafla ya ufunguzi wa Wiki hiyo iliyofanyika katika Ofisi za TANESCO Mkoa wa Temeke, Kurasini, Dar es Salaam, Mhandisi Babu amesema uwajibikaji, uzalendo na kujituma ni nguzo muhimu katika kuhakikisha shirika linaendelea kutoa huduma bora na zinazokidhi mahitaji ya wateja.

Amewataka wafanyakazi kuongeza juhudi na kwenda “Mbele Zaidi Kihuduma” kwa kubuni na kutekeleza njia bora zaidi za kuwahudumia wateja, huku wakizingatia weledi, uadilifu na kasi katika kushughulikia mahitaji na changamoto zao.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Lucia Renatus, amesema hatua ya ziada katika kutoa huduma siyo kufanya kazi yako tu bali kufanya zaidi ya kile ulichopangiwa kufanya kutoka kwenye wajibu na kuingia kwenye kujali mteja zaidi.

Amesema katika huduma kuna hatua tatu, huduma inayotarajiwa, huduma unayotoa na huduma ya ziada ambayo inayomshagaza na kumfurahisha mteja

Katika hafla hiyo, wakuu wa idara mbalimbali pamoja na wafanyakazi walieleza mipango na mikakati wanayoendelea kutekeleza katika maeneo yao ili kuhakikisha TANESCO inaendelea kutoa huduma bora, kwa ufanisi

Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 imebeba kaulimbiu isemayo “Mbele Zaidi Kihuduma.”