Kamishna wa Intelijensia ya Jinai, CP Charles Mkumbo ambaye ni muwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Ramadhan Kingai, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji CP Hamad Khamis Hamad pamoja na Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime wakiwasili katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Kamati ya Kudumu ya Ulinzi na Usalama (JPCDS) kati ya Tanzania na Msumbiji, unaofanyika katika Ukumbi wa Aga Khan Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 05, 2026.
Mkutano huo unalenga kujadili masuala ya ulinzi na usalama, kutathmini utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano iliyopita pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazovuka mipaka ya nchi hizo mbili. Picha na Jeshi la Polisi.

