Kuna wakati nunua tu, hata kama hukuwa na shida na kitu hicho. Na ikiwezekana, mnunulie hata yeye mwenyewe, hata kama ni mayai mawili.
Kuna watu wanazipambania familia zao kwa jasho na damu wakiwa katika umri mdogo, kwa sababu hawawezi kuiba wala kunyang’anya cha mtu. Wanatafuta riziki zao kwa njia halali, bila kumdhulumu mtu.
Kununua kwako si tu kwamba utakuwa umemsaidia katika harakati zake za kuisaidia familia yake, bali utakuwa pia umemtia moyo katika mapambano yake. Na kwa kufanya hivyo, naamini Mungu atakubariki zaidi.
Maisha yamebeba siri kubwa sana katika medani ya kupambania riziki. Ukimtazama huyo mwamba hapo, utagundua kuwa amebeba matumaini makubwa ya kuikomboa familia yake.
Mwamba amekataa kuuza ubingwa, kuiba wala kucheza kamari. Anaamini katika mapambano ya kutafuta riziki yake kwa njia halali.
Ipo siku tutarudi nyumbani, ikiwa tupo kwenye Range Rover au kwenye jeneza, lakini tutarudi nyumbani. Familia zimetutuma kupambana na kuhakikisha tunapeleka mkate nyumbani.
Hatupaswi kuonyesha machozi wala machungu tunayopitia, kwa sababu nyumbani kuna watu wanatutazama. Tukiruhusu machozi yatuanguke, tunaweza kuwakatisha tamaa.
Haya ndiyo maisha ya baadhi ya watu wanaopambana kila siku kutafuta riziki kwa njia halali. Kila hatua wanayopiga ina nyuma yake familia inayowategemea, na kila jasho wanalolitoa ni sehemu ya safari ya kuhakikisha wapendwa wao wanapata mahitaji yao.
Kwa hiyo, wakati mwingine usipuuze mtu anayekuja kwako kuuza kitu. Nunua hata kama hukupanga kununua. Huenda kile unachokiona ni bidhaa ndogo, lakini kwake kinaweza kuwa sehemu ya matumaini makubwa ya familia yake.
