.Na Sixmund Begashe, Moshi 

WIZARA ya Maliasili na Utalii kupitia Club yake ya Michezo, imeendelea kuwa gumzo kwenye Michezo ya SHIMIWI 2026 baada ya mkimbiaji wake Bw. Amandus Rutaihwa kuwatoa jasho la kutosha wazee wenzake kwenye mbio za wazee za Mita 100 kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi, Kilimanjaro. 

Bw. Rutaihwa ambaye aliwavutia wengi kwa kasi yake ya ajabu iliyotokana na aina yake ya ukimbiaji aliyoitambulisha kama ‘Kula vumbi’.

Pamoja na kushika nafasi ya 4 kwenye mbio hizo Bw. Rutaihwa ameupongeza uongozi wa SHIMIWI kwa kuweka mbio hizo kwa kuwa zinawasaidia wazee kupata hamasa za kufanya mazoezi hali inayoimarisha afya zao.