Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka, amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro, Bi. Husna Nyange, Ofisini kwake leo.
Kikao hicho kimelenga kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na TRA katika kuongeza uelewa kwa wananchi na wafanyabiashara wa Kilosa kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Katika mazungumzo hayo, wamejadili mikakati ya pamoja ya kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari, kudhibiti biashara holela na kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa wafanyabiashara, ili kuifanya Kilosa kuwa kitovu cha uwekezaji na biashara Mkoani Morogoro.
“Kodi zenu ndizo zinazojenga Kilosa yetu na Tanzania yetu. Ni wajibu wetu wote kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yetu.” – Mhe. Shaka.

