Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Komandi ya Ushirikishwaji wa Jamii katika Jeshi la Polisi Nchini, ACP Elisante Ulomi, na ujumbe wake kutoka Makao Makuu ya Polisi na Mkoa wa Morogoro, aliyeko wilayani Kilosa kwa ziara maalum ya kuimarisha uhusiano kati ya wananchi na Jeshi la Polisi katika masuala ya ulinzi, usalama na amani.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Jumanne, Septemba 30, 2026, Ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa.

