Na Sixmund Begashe, Moshi
TIMU ya Maliasi Sports Club ya mpira wa Pete KE imeaikandamiza timu ya Haki KE ya Tume ya Haki na Utawala Bora, magoli 41-7 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya Chuo cha Polisi (CCP) Moshi.
Timu ya Maliasili ilianza kwa kasi kubwa na kumalizia kwa kasi zaidi kutokana na ari iliyoletwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Bernard Marcelline na mashabiki wa timu hiyo kutoka viunga mbalimbali vya mji wa Moshi.
Akizungumza na wachezaji na mashabiki wa timu hiyo yenye wachezaji machachari, Bw. Marcelline pamoja na kuzipongeza timu zote za Club ya Michezo ya Maliasili zilizoibuka na ushindi, amewataka kuongeza juhudi ili kuendelea kushinda michezo inayofuata.
Aidha Bw. Marcelline amewasisitiza wachezaji hao kudumisha upendo na uhusiano mwema na wanamichezo wa timu nyingine ambao wote ni watumishi wa umma.

