Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Christopher Mwakibinga akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Katika kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora Wakala wa Vipimo Nchini (WMA) wanaendelea na utaratibu wa kuwafata wafanyabiashara kwenye maeneo yao lengo ikiwa ni kuwapa elimu sanjari na kuhakiki bidhaa.

Hayo yamebainishwa Septemba 03,2026 na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bw. Christopher Mwakibinga Wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao liliko kwenye maonesho ya 21 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Amesema pamoja na kuwafata wafanyabiashara kwaajili ya kuwapa elimu pia amewahimiza wananchi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatumia vipimo ambavyo vimehakikiwa na wakala wa vipimo.

“Vipimo vyetu vinatambulika kirahisi sana kwani tunaweka rakili na stampu yetu ambayo itaonesha bidhaa imekaguliwa hivyo wananchi wasitumie bidhaa ambayo imeuzwa bila kuwa na vipimo ambavyo vimehakikiwa na wakala wa vipimo”, Amesema Mwakibinga

Aidha, amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwakuzingatia Sheria,kanuni na taratibu kwakuongozwa na Dira ya Taifa ambayo imeanza kutumika Julai 01 mwaka huu

Amesema anaishukuru sana Serikali kwa namna ilivyowawezesha wao kama Wakala wa Vipimo na matokeo yameweza kuoneka ikiwa ni pamoja na kuwa washindi wa kwanza katika kundi la Taasisi za Serikali zinazoshughulika na udhibiti.

Mwisho alitoa rai kwa wafanya biashara kuendelee kutii sheria ya vipimo bila shuruti kwani kwakufanya hivyo wataweza kufanya shughuli zao vizuri.Wananchi wakipewa elimu