Kikosi cha Yanga SC kimepata matokeo yasiyoridhisha baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Aigles du Congo katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Yanga Day.

Katika mchezo huo uliolenga pia kuwatambulisha wachezaji wa kikosi hicho, Yanga SC ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake, Shalulile.
Hata hivyo, Aigles du Congo walirejea mchezoni na kusawazisha kupitia Talasi, kabla ya mchezaji huyo kuongeza bao la pili na kuipa timu yake ushindi wa mabao 2-1.

Matokeo hayo yanakuwa sehemu ya maandalizi ya Yanga SC kuelekea msimu mpya, huku benchi la ufundi likipata nafasi ya kutathmini uwezo wa wachezaji wake kabla ya kuanza kwa mashindano rasmi.