Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamekubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kenya Police katika mchezo wa Simba Day uliopigwa leo, Agosti 8, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Bao pekee la Kenya Police lilifungwa na Elvis Rupia dakika ya 90 ya mchezo.
Mchezo huo ulitumika maalum kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wa Simba SC kwa mashabiki wao.
