Na Mwandishi Wetu

WANASIMBA wamehitimisha hamasa ya Wiki ya Simba 2026 kwa kushiriki kuitandika ya Biryani (Ubwawa) ya nguvu iliyoandaliwa kwa ajili yao , ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha tamasha la Simba Day 2026 linalofanyika kesho.

Safari hiyo imeongeza hamasa miongoni mwa mashabiki wa Simba, ambao wameendelea kujipanga kwa siku hiyo muhimu inayotumiwa na klabu kuwakutanisha mashabiki pamoja na kutambulisha kikosi cha wachezaji kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Simba Day inatarajiwa kuambatana na burudani mbalimbali, huku macho ya Wanasimba yakielekezwa zaidi kwenye utambulisho wa kikosi kipya na mipango ya timu kuelekea msimu mpya.

Kwa Wanasimba, Simba Day 2026 ni zaidi ya tamasha, bali ni fursa ya kuonyesha upendo na kuipa timu hamasa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mashindano.