Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, katika hafla ya kuwaapisha viongozi wanne aliowateua hivi karibuni, leo tarehe 24 Julai 2026, Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Mhe. Valentina Andrew Katema kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, leo tarehe 24 Julai 2026, Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Mhe. Khamis Ali Simai kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, leo tarehe 24 Julai 2026, Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Dkt. Josephine Rogate Kimaro kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, leo tarehe 24 Julai 2026, Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na viongozi wanne aliowaapisha katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, iliyofanyika leo, tarehe 24 Julai 2026, Ikulu Zanzibar.

……….. 

ZANZIBAR, Julai 24, 2026 – Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha viongozi wanne aliowateua hivi karibuni, wakiwemo majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Hafla ya uapisho imefanyika leo Ikulu Zanzibar, ambapo Rais Dkt. Mwinyi amewataka viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, weledi na kuzingatia maslahi ya wananchi.

Viongozi walioapishwa ni Dkt. Mahadhi Juma Maalim ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, Mhe. Valentina Andrew Katema aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mhe. Khamis Ali Simai ambaye pia ameapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, pamoja na Dkt. Josephine Rogate Kimaro aliyeapishwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mansoura Mossi Kassim, pamoja na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa dini na wageni mbalimbali waalikwa.