WAZIRI wa Kilimo na mlezi wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Daniel Godfrey Chongolo (Mb) akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mwinyi.Ahmed Mwinyi alipofanya ziara yake wilayani humo leo.
Na Happy Lazaro, Arusha 
WAZIRI wa Kilimo na mlezi wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Daniel Godfrey Chongolo (Mb) amewataka  wananchi wa wilaya ya Arumeru kuendelea kulinda tunu ya amani ya Taifa, inayopelekea utulivu wa kufanya kazi za uzalishaji kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Waziri Chongolo ameyasema hayo leo wilayani Arumeru wakati akiwa.katika.ziara yake ya siku.moja ya kukagua miradi mbalimbali.
Aidha Waziri Chongolo  amewasili wilayani Arumeru na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi pamoja na viongozi wa chama na Serikali.
Katika ziara yake Waziri  Chongolo ameweza kukagua shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya KIA- Usa River,pamoja na  kutembelea mradi wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji Kipande- Nkoavere Kata ya Nkonrua, kuzindua mabweni mawili, madarasa matano na matundu nane ya Vyoo kwenye Shule ya Sekondari na baadaye kuzungumza na  wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika  eneo la Usa River .
Aidha Chongolo ameshukuru kwa mapokezi mazuri na kupongeza uongozi wa wilaya ya Arumeru kwa usimamizi mzuri wa shughuli za maendeleo unaowezesha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo na kusisitiza viongozi na wananchi kuitunza tunu ya amani ya Taifa la Tanzania inayoleta utulivu kwa maendeleo yao na Taifa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Mwinyi Ahmed Mwinyi ametumia fursa hiyo kumkaribisha Waziri Chongolo Arumeru wilaya yenye Halmashauri mbili za Arusha na Meru sambamba na kumhakikishia hali ya amani na utulivu iliyopo wilayani humo inayoruhusu wananchi kuendelea na shughuli zao za kulijenga Taifa pamoja na kumtaka kufurahia mandari  nzuri ya utalii iliyoambatana hali ya hewa chini ya mlima Meru, inayovutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi

Ziara ya Mhe. Chongolo mkoani Arusha imeanza Julai 22 na itahitimishwa Julai 25, 2026. Katika kipindi hicho, anatembelea wilaya za Karatu, Monduli, Arumeru na Arusha, ambapo anakagua miradi ya maendeleo, kusikiliza changamoto za wananchi na kutoa maelekezo yanayolenga kuongeza kasi ya maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi.