Timu ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Canada mabao 3-0 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora.
Mabao ya Morocco yalifungwa na Azzedine Ounahi aliyetikisa nyavu dakika za 50 na 82, huku Soufiane Rahimi akifunga bao la tatu dakika ya 90+7.
Kwa ushindi huo, Morocco imefuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia 2026, huku wenyeji wenza Canada wakiaga rasmi mashindano hayo
