Baada ya kusubiri kwa miaka minne hatimaye Simba SC imetwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kuichapa Azam kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba Zanzibar.
Wakati Simba inakabidhiwa kombe lake, lakini tukio la kushangaza wachezaji wa Azam pamoja na kocha Florent Ibenge hawakwenda kuchukua medali zao za ushindi wa pili.
Ubingwa huo unaifanya Simba kumaliza ukame wa kusubiri miaka minne tangu walipofanya hivyo mwaka 2021 na kupita kipindi cha ukame wa kuchukua makombe tofauti na ilivyofanya msimu huu chini ya kocha Steve Barker raia wa Afrika Kusini. Hili ni Kombe la tano la Simba la CRDB, lakini likiwa ni la nne tangu liliporejea.
Hata hivyo, rekodi imeendelea kuwabeba Simba ambapo kila ilipofanikiwa kufika fainali kwenye michuano hiyo imefanikiwa kuchukua ubingwa huo.
