

Mhandisi wa Umeme wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO), Aron Julius Munuo (wa pili kulia), akitoa elimu kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya umeme katika banda la kampuni hiyo, lililopo ndani ya banda la TANESCO, wakati wananchi walipotembelea Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Mhandisi wa Umeme wa Kampuni ya ETDCO Abuu Hamisi akitoa elimu ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya umeme katika banda la kampuni hiyo, lililopo ndani ya banda la TANESCO, wakati wananchi walipotembelea Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)

Wananchi wakielimishwa kuhusu utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya umeme katika banda la Kampuni ya ETDCO wakati wa Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, Dar es Salaam, kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2026.