Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab A. Katimba (Mb) ametembelea Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam, tarehe 1 Julai, 2026.

Aidha, Mhe. Katimba ameipongezea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushiriki kwenye Maonesho na kuendelea kutoa elimu na kusogeza huduma za Kisheria kwa wananchi.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inashiriki Maonesho ya Sabasaba yaliyoanza tarehe 28 Juni, 2026 na yanaendelea hadi tarehe 13 Julai, 2026 ambapo banda la Ofisi liko ndani ya Ukumbi wa Karume.