Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliyofanyika kwa njia ya Mtandao, leo tarehe 29 Juni 2026, Makamu wa Rais akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa.