Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) ambaye pia ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Alex Gehaz Malasusa baada ya kuwasili katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 24 Juni, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia video fupi kuhusu historia ya Hospitali ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) pamoja na ujenzi wa Jengo la Tiba Mionzi (Radiotherapy Unit) katika Hospitali hiyo, Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 24 Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipanda mti aina ya stafeli kama kumbukumbu ya uzinduzi wa Jengo la Tiba Mionzi (Radiotherapy Unit) katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC), Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 24 Juni, 2026.
